Nguli wa muziki wa kufoka nchini Marekani, Cardi B ametangaza rasmi juu ya nia yake ya kutaka kuhamia nchini Nigeria ikiwa vita kati ya Marekani na Iran itaanza.
Kutokana na machafuko yanayoendelea nchini Iran yakifuatiwa na mauaji ya Meja Jenerali wa taifa hilo Qasem Soleimani katika mji wa Baghdad nchini Iraq akiwa anatoka uwanja wa ndege
Siku chache baada ya kupumzisha mwili wa kiongozi huyo katika makazi ya milele, Iran ilitangaza hali ya hatari dhidi ya taifa la Marekani ambalo ndilo limehusishwa moja kwa moja katika mauaji hayo baada ya kutuma ndege zisizo na rubani na kumshambulia kiongozi huyo pamoja na wasaidizi wake.
Licha ya Iran kutangaza hali ya hatari na kuweka vitisho dhidi ya Marekani bado Rais wa taifa hilo Donald Trump, amesema kupitia ukurasa wake wa twitter kuwa yeye haogopi chochote na endapo Iran wataendelea kutoa vitisho na kujaribu kushambulia taifa au mali yoyote ya taifa hilo basi hatosita kujibu mapigo hayo kwani taifa la Marekani lina silaha za kijeshi za kutosha tena zenye gharama sana.
Kufuatiwa na kauli aliyoitoa Rais Donald Trump, baadhi ya wasanii wameonyeshwa kukerwa na kauli hiyo na kutangaza kutafuta uraia katika nchi zingine zenye amani na utulivu.
Miongoni mwa wasanii waliotoa kauli ya kutaka kuhama nchini Marekani ni nguli wa muziki wa kufoka nchini humo mwanadada Belcalis Marlenis Almanzar, Alimaarufu kama Cardi B ambaye ametangaza kupitia katika ukurasa wake wa Twitter nia yake ya kutafuta uraia nchini Nigeria.

Pia Cardi B aliweka chapisho lililonuonesha mumewe akiwa katika mavazi ya buluu yenye asili ya Nigeria huku akiahidi kuendelea kuwashawishi wasanii wenzake, akiwemo mume wake kutoka katika kundi la Migos ambaye ni Kiari Kendrell Cephus, alimaarufu kama Offset kuhamia nchini Nigeria pamoja naye.

Hapo awali, kumekuwepo na matukio mengi yanayohusisha wasanii wa marekani kuhitaji kutafuta uraia wa nchi zingine hususani za kiafrika, miongoni mwa wasanii hao akiwemo mwigizaji mkubwa kutoka Uingereza Idris Alba, ambaye mapema mwaka 2019 aliomba na kufanikiwa kupata uraia wa Sierra Leone. Pia muigizaji na mwimbaji wa muziki wa kufoka alimaarufu kama Ludacris naye aliamua kuomba uraia nchini Gabon ili kuwa pmoja na familia yake.
@miramagazinesupdates