Mchoro wa Monalisa ni moja kati ya michoro mingi ambayo ni maarufu duniani, Mchoro huu uliweza kuchorwa na mwanasayansi pia mchoraji Leonardo da Vinci katika karne ya 16.

Pia mchoro huu unajulikana kama La Gioconda ambapo maana yake ni mwanamke mchangamfu katika lugha ya kiitaliano.  na kwa sasa mchoro huu unapatikana katika makumbuso ya Louvre huko Ufaransa.

Mchoro wa Monalisa ulianza kujipatia umaarufu baada ya kuibiwa mwaka 1911.

Mchoro huu wenye gharama kubwa sana ulijipatia umaarufu wake katika uso wa dunia baada ya kuibiwa mnamo Tarehe 21 Agosti 1911 kutoka katika Makumbusho ya Louvre iliyoko Paris, Ufaransa.

Kutokana na maelezo ya mwandishi Seymour Reit anasema kwamba

mchoro huu uliibiwa siku ya Jumatatu asubuhi lakini haikugundulika kuwa umeibiwa mpaka pale ilipofika siku ya Jumanne mchana

Baada ya taarifa kutolewa katika vyombo vya usalama hasa katika kitengo cha taifa cha uchunguzi wa makosa ya kiuhalifu, Wakaguzi wakiongozana na polisi walifika katika eneo la tukio kwa ajili ya ukaguzi.

Baada ya mahojiano ndipo ilipogundulika mchoro wa Monalisa uliibiwa siku moja kabla ya wao kugundua kuwa umeibiwa.

Reit anaendelea kwa kusema kuwa

habari hizi ziliishangaza dunia, bila shaka ulikuwa na maana kwa dunia nzima na hivyo iliandikwa katika kurasa za kwanza za kila gazeti kubwa duniani.

Baada ya kuibiwa kwa mchoro wa Monalisa watu wengi mashuhuri katika sanaa walianza kutunga nyimbo na kuandika mashairi yaliyohusiana na upotevu wa mchoro wa Monalisa na hii ilipelekea kuanza kukua kwa umaarufu wa Monalisa

Kwa muda wa miaka miwili mchoro wa Monalisa ulitafutwa na haukupatikana lakini ilipofika  mnamo November 1913 mchoro wa  Monalisa ukapatikana tena

Nani aliiba mchoro wa Mona Lisa mwaka 1911?

Vincenzo Peruggia alizaliwa mwaka 1881 huko Dumenza Varese nchini Italia ndiye muhusika mkuu anayefahamika kama mwizi wa mchoro wa Mona lisa, baada ya kukamatwa katika mahojiano alisema kuwa,

Soma pia Penzi la wakala wa Giza; Ep 02.
Soma pia Cardi B atangaza rasmi kujaza fomu za kuomba uraia nchini Nigeria.
Soma pia Je Wajua?: Nchi mbili zilizowahi kutumia bendera zinazofanana

Aliingia ndani ya Makumbusho mapema ikiwa ni saa moja asubuhi kupitia mlango ambao wafanyakazi wa Louvre huwa wanapitia, anasema kuwa alivaa nguo ambazo zinaendana na wafanyakazi wa Louvre hivyo ilikuwa ngumu kwa wao  kumtofautisha.

Vincenzo anasema kuwa baada kuingia chumba ambacho mchoro wa Mona Lisa ulihifadhiwa aliuondoa ukutani kisha akaugubika kwa kitambaa na kuubana katika kwapa la mkono wake na kuondoka, akipitia mlango ule ule aliotumia katika kuingia.

Ndani ya miaka yote miwili aliuficha mchoro huo katika nyumba ambayo alikuwa akiishi huko Florence, Italia.

Baada ya kukaa na mchoro kwa muda wa miaka miwili aliamua kumpigia simu Alfredo Geri, mmiliki wa Jumba ya kuhifadhia Picha na Michoro ya Kisanaa huko Florence.

Vincenzo alifanya hivyo akitegemea kupata malipo lakini Alfredo hakufanya hivyo badala yake aliuchukua mchoro kisha akautunza na kupiga simu polisi ili kutoa taarifa juu ya kupatikana kwa mchoro wa Mona Lisa nchini Italia.

Baada ya Polisi kufahamu tukio hili walimsaka Vincenzo Peruggia hadi walipompata akiwa hotelini kwake, Vincenzo alipelekwa Jera na aliachiliwa baada ya kulitumikia jeshi la italia katika vita vya kwanza vya dunia.

Hivi sasa mchoro wa Mona Lisa umehifadhiwa katika makumbusho ya Louvre, Paris nchini Ufaransa, umekuwa mchoro namba moja kwa umaarufu duniani ambapo hupata watalii zaidi ya Milioni sita kwa mwaka kwenda kuutazama mchoro huo

Miongoni mwa michoro mingine ambayo ni maarufu duniani ni

The Last Supper uliochorwa na Leonardo Da Vinci mmoja kati ya wachoraji mashuhuri alichora mchoro huu mnamo  karne ya 15. Mchoro huu unaonyesha Yesu na wanafunzi wake wakila chakula cha jioni

the_last_supper-1024x556

The Creation of Adam, uliochorwa mnamo mwaka 1508 mpaka 1512 na mchoraji mashuhuri Michelangelo

The_Creation_Of_Adam

The persistence of Memory uliochorwa mnano mwaka 1931 na mchoraji wa Kihispania Salvador Dali

The_Persistence_of_Memory

Tafadhali kwa kupata makala kemkem za aina hii usiache kusubscribe/ kufollow mira magazines, kwa kufanya hivyo utakuwa mmoja kati ya wengi wanaopokea makala zetu kwa wakati