Ilipoishia…

Alaaaas!!! Nilikuwa naota oooh…. Asante Mungu ni heri nimeota tu ni heri haijawa kweli  aaah lakini kwanini ndoto mbaya hivi mmh bila shaka kuna jambo baya linakuja mmh Mungu epushia mbali…

Endelea sasa…..

Asubuhi na mapema Ndaki aliamka kisha akafanya kazi zake za nyumbani kama ilivyo ada, tayari alishajua kuwa mama yake Bi Fatma ameshaondoka na kwenda kazini, hivyo alipomaliza kazi zake alijiandaa na akaamua kuondoka kuelekea chuoni alikokuwa akisoma.

Njiani alitembea haraka huku wimbo uliomsindikiza ikiwa ni ndoto yake ya jana usiku, kuna muda alijisemea moyoni aah lakini yule msichana alionekana kuwa mremboooo!! japo sijaiona sura kamili!! Mmh ila hata sauti yake ilivutia mno!! Aaah lakini si ndo aliniua mwishoni haha hawa wasichana buana!!!…….

Aliendelea na safari yake huku akiwaza na kuwazua aliachia tabasamu zito pale alipokumbuka kuwa yale yote yaliyomkuta ilikuwa ni ndoto tu.

Punde alifika chuoni kwao, Pewagia International University (PIU).  Alionesha kitambulisho chake getini kisha akaruhusiwa kuingia ndani, alitembea kuelekea upande wenye kibao kilichoandikwa Pewagia Law School (PLAS), ghafla mawazo yake yalitawanywa na sauti aliyosikika kutoka kwa rafiki yake aliyeitwa Abdul.

“oyaaa mzee nimekuita muda mrefuuu sana halafu umenikausha tu dah!” Abdul Alisema

“aaaaah!! Acha utani Faza mbona sijakusikia hata kidogo” Ndaki alijibu huku akicheka,

“Aaah sawa! buana nyie washua ndivyo mlivyo mkiitwa hata mara mia huwa hamsikii mpaka tuwafuate” Abdul alijibu huku akimshika Ndaki mkono na kuelekea darasani kwa pamoja.

Wote walikuwa wakichukua mafunzo ya sheria na walikuwa wameshafikisha mwaka wa pili, walienda kwa haraka sana kwani walijua kuwa wameshachelewa darasani na Profesa alishaanza kufundisha.

Soma hapa Penzi la wakala wa Giza; Ep 01
Soma hapa Penzi la wakala wa Giza; Ep 02.

Walipofika walipitia mlango wa nyuma na kuingia darasani, kama ilivyo kawaida Ndaki aliekea kiti chake na kuketi, nyuma yake palikuwa na kiti kisicho na mtu yeyote, Profesa alikuwa akiendelea kufundisha na wanafunzi walikuwa kimya kumsikiliza.

“Mr. Simba you’re always late, you never changed” Profesa alisema akimuambia Ndaki juu ya tabia yake ya kuchelewa darasani.

Ndaki alisimama na kutaka kujitetea lakini Profesa alikataa kisha akamuambia aketi chini bila kumruhusu kusema neno lolote la utetezi, alimueleza kuwa amechoshwa na tabia yake ya kuchelewa darasani na hivyo anatakiwa kubadilika.

Alifundishwa kwa muda kisha akauliza swali lililokuwa na mtego ndani yake japo ni somo la Sheria bado swali hilo lilihitaji ujanja kidogo hili uweze kulijibu ipasavyo.

“Suppose I have a company, and I want to voluntarily wind up my company as it has more liabilities than assets? Is there any law that stops me from doing so?” (Tuseme nina kampuni, na ninataka kuifunga kampuni yangu kwa hiari kwani ina madeni zaidi kuliko mali? Je! Kuna sheria yoyote ambayo inanizuia kufanya hivyo?) Profesa aliuliza swali lillilogonga vichwa vya wanafunzi wake

Wanafunzi wote walikaa kimya wakitafakari swali waliloulizwa na Profesa wao, walitumia kama dakika kumi wakilijadili swali hilo bila kupata majibu, ambayo waliona yangempendeza Profesa wao, ndipo Ndaki alipoonyosha mkono juu akitoa ishara ya kutaka kujibu swali hilo.

“Wow seems Mr Simba has got something to tell the class, you’re welcome” (“Wow inaonekana Mr Simba ana jambo la kutuambia, karibu”) Profesa huku akionyesha hali ya mshangao alimkaribisha Ndaki kutoa majibu ya swali alilouliza.

“Actually the company will never progress if it has more liabilities than assets, and it will only end up being bankrupt, I don’t think if there will be anyone to stop it when you decided to wind it up” (kiukweli kampuni haiwezi kuendelea kama ikiwa ina madeni mengi kuliko mali, na itaishia tu kufilisika, sidhani kama kutakuwepo na mtu yeyote atakayezuia kufungwa kwa kampuni yako) Ndaki alimaliza kutoa jibu lake.

“Mmmh!! Good try Mr Simba, the whole class is amazed you were never expected to give a good answer like that, but yet I need the excellent answer from all of you!! (“Mmh! Umejitahidi Mr Simba darasa zima limeshangazwa, hukutegemewa kutoa jibu zuri kama hilo, japo bado nahitaji jibu zuri Zaidi kutoka kwenu kwa pamoja”) Profesa aliongea huku akitabasamu kwani aligundua kuwa amewapa swali kiboko na limewapiga hadi vigongo wa darasa alitambua kuwa hakuna ambaye angeweza kutoa jibu stahiki kwa swali lake.

Ghafla ilisikika sauti kutoka mlangoni “The excellent answer you seek is here professor” (Jibu zuri Zaidi unalolihitaji lipo hapa Profesa) Sauti ya msichana mmoja ambaye alionekana mgeni katika darasa hilo aliongea kutokea mlangoni.

Darasa zima lilibaki mdomo wazi kama wanapiga miayo, wavulana wa darasa lile tayari mioyo yao ilishaanza kwenda mbio, walishindwa kabisa kuvumilia udenda uliwatoka kwa uzuri alionao binti yule, Profesa alilliona jambo hili akaamua kuwashtua wanafunzi wake kwa kumpa ruhusa binti yule aendelee kuongea…

“Such a question can be attempted with The Companies Act, which is Act No 12 of 2002 states that, where it is proposed to wind up a company voluntarily, the directors of the company at a meeting of the directors must make a declaration in the prescribed form to the effect that they have made a full inquiry into the affairs of the company, and that, having so done, they have formed the opinion that the company will be able to pay its debts in full within such period not exceeding twelve months from the commencement of the winding up as may be specified in the declaration so the directors are the ones’s to pull the company of the risk”

(Swali kama hili linaweza kujibiwa na Sheria ya Makampuni, ambayo ni Sheria ya 12 ya 2002 inasema kwamba, inapopendekezwa kufunga kampuni kwa hiari, wakurugenzi wa kampuni hiyo katika mkutano wa wakurugenzi watatoa tamko katika maagizo yaliyowekwa, fomu ya kuhakikisha kwamba wamefanya uchunguzi kamili juu ya maswala ya kampuni, na kwamba, wakiwa wamefanya hivyo, wameunda maoni kwamba kampuni itaweza kulipa deni lake kamili katika kipindi kama hicho kisichozidi miezi kumi na mbili ya mwanzo, kama inaweza kutajwa katika tamko. Kwa hivyo wakurugenzi ndio wanaoweza kuitoa kampuni katika hatari)

Alilitoa jibu hilo kwa ufasaha na misingi ya kisheria kabisa, alipigiwa makofi na darasa zima huku kila mmoja kichwani mwake akitafakari sauti nyororo ya msichana yule jinsi ilivyopenya ndani ya masikio yake na kusababisha mtetemo katika mishipa ya upendo moyoni.

Japo haikuwa hivyo kwa Ndaki, moyo wake ulienda mbio zaidi ya wengine alihisi kupooza ndani ya muda mfupi tu, alikaa kimya bila kupiga makofi akitafakari sauti ya msichana yule jinsi ilivyofanana na sauti aliyoisikia katika ndoto yake jana usiku.

Muda wote alikaa makini akiitazama midomo ya msichana yule kwani rangi zilizopakwa zilifanana kabisa na za midomo ya msichana aliyemuota jana usiku.

“aaah!!! Lakini hata midomo hufanana haina noma…!!” alibaki kujisemea hivi ili ajifariji na kujiondolea hofu aliyo nayo moyoni mwake. Alijisemea moyoni mwake kuwa wacha asogee ajitambulishe nitamjua tu kama ndiye au siye!.

Profesa naye alitikisa kichwa chake na kutoa tabasamu, kisha akatoa ishara kuwa hilo ndilo jibu alilokuwa akilihitaji kutoka kwa wanafunzi wake, aliamua kumkaribisha mwanafunzi yule darasani na ajitambulishe yeye ni nani na anatokea wapi.

Maneno hayo yalimfanya Ndaki kuongeza umakini maradufu ili mradi asikie binti yule ni nani na anatokea wapi, ili ajiridhishe ndani ya moyo wake kuwa ndiye au siye yule anayemfikiria kichwani mwake.

Binti yule alitembea kwa madaha kama mlimbwende wa dunia akielekea mbele ya darasa, hakika kwa wakati ule alikuwa tayari ameshaiteka mioyo ya wavulana wengi katika darasa lile, sheria waliyoisoma ilihama kwa muda, vichwa vyao viligubikwa na uzuri alionao binti yule.

Pua zao zilivuta pumzi iliyojawa na marashi yake, kila alipotembea hatua moja kwenda mbele shepu yake ilizidi, ilionekana vizuri katika gauni jekundu alilovaa, hakika lilimpendezea mno.

Rangi yake kama Mjamaika ndiyo ilizidi kuchanganya akili za wengi, nywele zake ndefu alizoziacha zikimwagika mpaka mgongoni mwake ziliruka ruka kila alipopiga hatua, wavulana wengi walibaki kimya kama wamerukwa na akili, ni miguno ya wivu na sauti za kusonya tu ndizo zilizosikika kutoka kwa wasichana kwani walijua tayari wameshaibiwa wavulana wao.

“aaaamh am Nelya Adeleke from… Nigeria… I’ll be here in Pewagia International University persuing my Law degree course…” (aamh jina langu ni Nelya Adeleke natokea Nigeria nitakuwa hapa Pewagia International University nachukua shahada ya Sheria. Msichana yule alijitambulisha mbele ya darasa

“where Nigeria!! Why Nigeria!!” Ndaki alijikuta akitamka kwa sauti kubwa darasani watu wote waligeuka na kumtazama, alibaki akijishangaa ni kwanini ametamka bila kupanga kutamka maneno yale.

Msichana Nelya kutoka Nigeria alibaki akimuangalia Ndaki kisha akatabasamu tu wala hakuonesha kuchukia, darasa zima likatabasamu na kutoa vicheko hafifu wakamuona Ndaki kama mtu wa kwanza kupagawa na uzuri wa binti yule.

Profesa aliwanyamazisha, kisha akamueleza aende kuketi nyuma ya Ndaki ambako ndipo palikuwa na kiti tupu kisichokaliwa na mtu yeyote, akilini mwake Ndaki alibaki akijuliza kwanini Profesa hakushangaa kuhusu ugeni wa mwanafunzi katikati ya kipindi chake, na badala yake akamkaribisha vizuri tena kwa furaha wakati haikuwa kawaida ya Profesa wao.

Nelya alitembea kwa maringo huku macho ya wavulana wengi yakimsindikiza mpaka sehemu alipoenda kukeki, nyuma ya Ndaki, alifika akaketi na kutulia.

Wakati huo Ndaki alikuwa na mawazo mchanganyiko huku akijiuliza mambo mengi kuhusiana na ndoto yake ya jana ambapo alipelekwa Nigeria bila ya kutarajia na alitakiwa kuuawa, aligeuka nyuma na kumuangalia Nelya ambaye kwa sasa alishatoa kompyuta mpakato (laptop) yake aina ya Macbook na kuweka mezani kisha akaifugua.

“Nelya will join Mr Simba’s group discussion, from today onward…” (Nelya utajumuika katika kundi la Mr Simba kuanzia leo) Profesa alisema akiliambia darasa.

“but why Professor…. Why she’s gonna join my group… my group is full Sir” (lakini kwanini Profesa… kwanini ajiunge katika kikundi changu hali likiwa limejaa wanachama?) Ndaki alijaribu kwa kujitetea kuwa kundi lake lilikuwa limejaa watu tayari.

“No, Mr Simba… Nelya will join your group…. End of the discussion” (hapana Mr Simba…. Nelya atajiunga na kikundi chako… mwisho wa majadiliano) Profesa alisema kwa ukali kidogo.

Baada ya dakika chache Profesa aliamua kuacha kazi ya majadiliano kisha akaondoka, Ndaki aliona changamoto imeshaanza, baada tu ya Nelya kujiunga katika kikundi chake kwa ajili ya masomo, moyoni mwake alijisemea nitawezaje kumuongoza mtu kama huyu ambaye simfahamu kwa chochote daah!!… alipiga moyo konde akijiambia kuwa yeye ni mwanamume hawezi kushindwa kirahisi hivyo.

Ndaki aliamua kuwakusanya wana kikundi wenzake na kuwaomba   waende darasa linaloitwa Block B kwa ajili ya majadiliano ya swali aliloacha Profesa, wote walikubali.

Walitembea taratibu wakielekea katika hilo jengo, Nelya alikuwa wa mwisho kutoka darasani alikaa nyuma akiwafuata wenzake, alifanya hivyo ili kuficha aibu alizonazo kwani kila mtu alikuwa akimtazama yeye na kwa kuuchunguza uzuri alionao.

Walipofika Block B waliketi katika viti na hapo ndipo Ndaki alipofungua  majadiliano yao kwa kumtambulisha Nelya kuwa ni miongoni mwao, Punde katibu wa kundi hilo aitwaye Sophia akadakia kumkaribisha Nelya huku akiachia tabasamu mwanana, mwanya wa Sophia katikati ya meno yake ulionekana sawia.

Jambo hili lilimfurahisha sana Nelya, aliamua kuinuka mahala alipoketi na kuwashukuru wote kwa pamoja aliongea maneno machache kwa lugha ya kimombo cha Kinigeria, aliongea kwa ustadi wa juu sana Ndaki alibaki akiziangalia lipsi za Nelya jinsi zikivyocheza.

Ingawa hakuwa na vigezo vya kutosha kujiridhisha kuwa Nelya ndiye msichana aliyemuota jana lakini alijiuliza kwanini jambo hili linaingiliana sana na ujio wa Nelya?.

Nelya alimaliza kuongea kisha akaketi katika kiti chake, walimpigia makofi kwa utambulisho wake katika kikundi chao,

Ndaki aliwanyamazisha baada ya kuona utulivu unapungua na kuchukua swali na kuliweka mezani tayari kulishambulia. Wote walikaa kitako kusubiri kiongozi aanzishe mada.

Ndaki alilisoma swali kwa makini na baada ya kulielewa alianza kuwaeleza wenzake maana na jinsi ya kujibu swali hilo, aligawa kazi ya kufanya kila mmoja na chake  alipofika kwa Nelya alisita kumpa alitamani angemwacha kwanza mpaka azoee chuo.

Nelya alitoa ishara ya kuonesha kuwa asingependezwa endapo asingepewa kazi ya kufanya kwa siku hiyo alisisitiza ingawa walimkatalia lakini hakujali alitamani sana kufanya kazi ile, Ndaki hakuwa na hiyana aliamua kumpa swali kisha akamuambia kuwa endapo atashindwa mahali basi asisite kumtafuta wa msaada Zaidi.

Baada ya kumaliza kupeana kazi Ndaki aliamua kuwaruhusu kila mmoja angeweza kuendelea na shughuli zake, wote waliinuka kwa pamoja na kuagana kisha kuondoka Ndaki alibaki peke yake akiwa ameketi macho yake yote yalikuwa mgongoni mwa Nelya.

Alimtazama vilivyo na asipate jibu lolote aliishia kusema tu “ipo siku nitajua tu maana ya ile ndoto…” Nelya alitembea kwa maringo sana kisha akatokomea..

Akiwa anakusanya vitabu vyake tayari kwa kuondoka, Ndaki alishangaa kuona funguo katika begi lake la mgongoni, hakuweza kujua ni funguo za nani, akaamua kuzitoa humo alipozitazama kwa makini alitambua kuwa ni funguo za gari. Alishangazwa kuona funguo kama zile kwani maishani mwake hakuwahi ona funguo zenye rangi ya shaba.

Hali hii ilimtia woga sana kwani anakumbuka mazingira ya kwenye ndoto yake yalitawaliwa na rangi ya shaba pia. Alitazama pembeni hakuona mtu yeyote, alitazama nyuma yake wala hakuona mtu alibaki ameshaangaa imekuwaje funguo za gari tena za kifahari amezikuta katika begi lake?.

Baada ya kuwaza na kuwazua kwa muda mfupi aliazimia kuondoka nazo bila ya kujali nani ni mmiliki wa funguo hizo, alitembea hatua chache ghafla alipoufikia mlango aligongana uso kwa uso na Nelya, moyo wake ulipiga Paaa!! Alishindwa la kufanya nguvu zilimwisha.

Ndaki akiwa ameegemea ukuta alishindwa la kufanya, saa hii aliuona uzuri dhahiri wa Binti mrembo Nelya aliyaangalia macho ya Nelya kwa ukaribu zaidi, ndipo alipogundua kuwa Nelya alionyesha kuwa na hofu moyoni mwake huku pumzi zao zikitoka kwa shida sana

“Please Ndaki..  have you….have you.. Seen my keys?!! My car keys…” (Tafadhari Ndaki…. Umeziona..umeziona funguo zangu… funguo za gari) Nelya aliuliza huku akiwa amejawa na wasiwasi sana

Please answer me Ndaki..  the  silver keys… have you seen them please” (Tafadhari   nijibu Ndaki.. ni za shaba umeziona tafadhari) Nelya aliendelea kuuliza.. akiwa amejawa na hofu sana

Ndakia alibaki kimya tu bila ya kusema neno lolote kijasho taratibu kilianza kumtoka pumzi yake ilikuwa ikitoka taratibu sana, akilini mwake alijua kuwa ni kweli funguo ameziona tena anazo katika mfuko wake,  lakini imekuwaje mpaka amezikuta ndani ya begi lake wakati muda wote alikuwa nalo mwenyewe mgongoni pake.

Alishindwa kutoka jibu la haraka alibaki akifikiria nini cha kujibu, uzuri wa Nelya ambaye sasa alikuwa ameshasogea karibu ya kifua cha Ndaki nao ulizidi kumchanganya na kumfanya awe bubu kabisa….

Itaendelea……