Katheryn Elizabeth Hudson almaarufu kama Katy Perry (35) amefunguka kuhusiana na mambo ya thamani ambayo amejifunza katika tasnia ya muziki.

Nguli huyo wa muziki wa Pop nchini Marekani ameeleza njia tofauti tofauti anazotumia katika kuwanyamazisha mashabiki ambao wanamsema vibaya katika mitandao ya kijamii kuhusiana na maisha yake ndani na nje ya muziki wake.

Akizungumza hayo katika American idol amesema kuwa anaamini katika tiba, anaamini katika tafakari, anaamini katika kujipenda na kuwa mwangalifu.

Malkia huyo wa muziki anayetamba kwa wimbo wa Never really end, aliendelea kusema kuwa kitu ambacho mtu alinambia na kikabadilisha maisha yangu ni kwamba, hakuna ambaye anaweza kukufanya uamini jambo fulani kuhusu wewe mwenyewe, ambalo hukuwahi kuliamini kabla.

Soma: Katy Perry adondosha chozi ‘American Idol’

Soma: Cardi B atangaza rasmi kujaza fomu za kuomba uraia nchini Nigeria.

Hivyo endapo mtu atakuambia kuwa wewe ni mnene, mbaya na ikakuhuzunisha, mmh! kwani ulishawahi kujifikiria kuwa upo hivyo?, unatakiwa kufikiri zaidi ya hapo.

Ikumbukwe kuwa Katy Perry akiwa kama jaji, amejiunga na American Idol mwaka huu ikiwa katika msimu wa 16 huku akiambatana na majaji wengine ambao ni Lionel Richie 70 pamoja na Luke Bryan 43.

Chanzo Hollywoodlife.com