Je Wajua: Tumbili kutoka Afrika Kusini aliyefahamika kwa jina la Jackie aliwahi kushiriki katika mapigano ya vita ya kwanza ya Dunia (WWI)?.

Baada ya mapigano kuisha alitunukiwa medali ya ushirika mzuri akiwa vitani, kisha akapandishwa cheo na kuwa Corporal.

Maajabu ya Tumbili huyu yalianzia mwaka 1915, baada Bw. Albert Marr kumkuta tumbili asiye na makazi maalumu akiwa shambani kwake anatangatanga, ndipo akaamua kumchukua na kwenda nae nyumbani kwake na kumpa mafunzo ya kuishi kama binadamu.

Baada ya tumbili huyo kuelewa vizuri mafunzo hayo ndipo akapewa jina la Jackie na kufanywa kama mmoja kati ya wanachama wa familia ya Bw Albert Marr

Baada ya muda kupita aliyekuwa mlezi wake Albert Marr mkazi wa Pretoria, Afrika Kusini kuamua kujitolea kushiriki katika vita ya kwanza ya dunia.

Alipopelekwa Jeshini Albert Marr alipatiwa cheo cha Private (PTE), mwenye namba 4927 na alipangiwa kushiriki vita hiyo katika mapigano dhidi ya Ufaransa.

Albert hakupenda kushiriki vita hile bila ya kuwa na Tumbili wake ambaye alimpenda sana, hivyo aliomba ruhusa ya kwenda vitani huku akiambatana na tumbili wake, akakubaliwa.

Baada ya Jackie kukubaliwa kujiunga na jeshi naye alipewa cheo cha private kama ilivyokuwa kwa mlezi wake.

Alishonewa mavazi ya kijeshi kama ilivyokuwa kwa wanajeshi wengine ambao ni binadamu kisha naye akapatiwa mafunzo pamoja nao na hatimaye akaingia uwanja wa vita kupambana pamoja nao.

Tumbili (Jackie) mwanzoni hakupewa heshima wala nafasi kubwa alipokuwa vitani, lakini kutokana na umahili wake katika vita kuanza kuoekana alianza kuthaminiwa.

Soma pia :Blanche Monnier: Binti aliyefungwa kwa miaka 25 ndani ya chumba chenye giza.

Je Wajua? Mchoro wa Monalisa ulipata umaarufu duniani baada ya kuibiwa kwake

Alipokuwa vitani Jackie aliweza kuwaburudisha wanajeshi waliopigana vita jambo hili likwasadia wanajeshi kupata nguvu na fuaraha iliyosaidia kupandisha morali katika uwanja wa vita hivyo Jackie akaaminika kama mwanajeshi aliyesaidia kupandisha morali mwanajeshi wenzie katika uwanja wa vita.

Jackie (tumbili) aliweza kufuata maagizo yote aliyopewa na wakuu wake alipokuwa vitani, ikiwemo kutoa heshima (salute) kwa wakuu wake kila mara walipopita karibu yake.

Vita vikiwa vinaendelea Jackie alijaribu kukusanya mawe na kujenga uzio ambao ungemzuia asipatwe na madhara ya vita,  kwa bahati mbaya Jackie (tumbili) akiwa anaendelea kujenga uzio wake bomu lilipiga karibu yake jambo ambalo lilimsababishia kupata majeraha ya bega na mguuni.

Kwa jinsi alivyoumia vibaya madaktari wa kivita walishauri Jackie awaishwe zahanati kwa matibabu kwani walifikiri kuwa mguu wake ulitakiwa ukatwe, lakini Jackie aligoma kupelekwa zahanati mpaka atakapomaliza kujenga uzio wake kisha ajifiche.

Kwa kitendo hiko cha kishujaa alichokifanya katika uwanja wa vita Jackie alizawadiwa medali na kupandishwa cheo kutoka Private mpaka kuwa Corporal.

Tarehe 11 Novemba 1918 ndio ukawa mwisho wa Albert Marr pamoja na Jackie kushiriki katika mapigano ya vita hiyo ambapo Jackie alipelekwa Uingerezza kwa mapumziko akiambatana na mlezi wake.

Jackie aliweza kupata umaarufu mkubwa sana katika magazeti ya Uingereza kama shujaa wa vita

Ilipofika Februari 14, 1919 Jackie na Albert Marr walipewa jukumu la kufanya kazi msalaba mwekundu ya kukufanya fedha kwa ajili ya matibabu tya wanajeshi wanaopambana katika vita.

Walifanya kazi hii vizuri na kukusanya kipato kikubwa sana katika shirika hilo safarin yao ilifika ukomo Aprili 24, 1919 baada ya kurudishwa nchini Afrika Kusini akiwa na mlezi wake Marr.

Akiwa anaruhusiwa Jackie alizawadiwa  fomu ya kuajiriwa kazini, pia fedha za kujikimu (pensheni).

Waliporejea nchini Afrika Kusini huko walipokelewa kwa heshima ya kijeshi na hapo Jackie na mlezi wake walizawadiwa tena medani iliyoitwa The Pretoria’s service medal.

Mauti bila Huruma yalimfika Jackie Mei 1921, katika ajali ya moto nyumbani kwao, naye Marr aliishia mpaka alipofariki  mnamo 1973 akiwa na miaka 84.