NYOTA wa muziki wa R&B nchini Marekani, Camila Cabello aeleza jinsi anavyofundishwa kupiga gitaa na mpenzi wake huku wakiwa kizuizini kuepukana na ugonjwa na Corona.

Mwimbaji huyo anayetamba kwa wimbo wa ‘Havana’ ameonyesha furaha yake kujifunza mambo mapya akiwa kizuizini na mpenzi wake Shawn Mendez.

Camila hivi karibuni ameweka picha yake katika ukurasa wake wa instagram iliyomuonesha akiwa amefunika jicho lake moja kwa gitaa huku akiambatanisha na maneno yaliyosomeka “Shawn ananifundisha, nami namfundisha Kihispania”

Tangu kutolewa kwa agizo la kila mmoja kukaa kizuizini katika baadhi ya nchi za ulaya na Marekani, nyota hao wawili wamekuwa wakitumia kurasa zao za instagram na twitter kama njia ya kuwasiliana na mashabiki zao.

Camila na Shawn wamesisitiza kuutumia muda wakiwa kizuizini kama muda wa kufurahi na mashabiki zao ambapo tarehe 20 Machi walishea video yao wakiwa wanatumbuiza katika tamasha la Global Citizen’s Together at Home Series iliyokuwa ikifanyika kwa njia ya mtandao

Video yao iliambatanishwa na maneno yaliyosomeka “Tutaimba nyimbo chache leo, kwasababu haitakiwa kujisikia upweke hata kama unaishi katika kizuizi”.