Msanii wa muziki wa Hip Hop nchini Emmanuel Elibariki maarufu kama Nay wa Mitego ameanika sababu ambazo zimemfanya msanii mwenzake Roma kukimbia nchini

Hivi karibuni Nay ameandika kupitia ukurasa wake wa Instagram maneno ambayo yamekuwa kama majibu kwa Roma Mkatoliki kutokana na ushauri ambao aliuotoa.

“Mpendwa Roma wewe ni mshikaji wangu sana, ila kuna wakati nadhani unajitoa ufahamu sijui. kwamba wewe unaimba nyimbo ambazo bimkubwa akisikia hawezi kupanick wala kupanikishwa na watu baada ya wimbo kuzua mijadala kwanza umekimbia nchini kwasababu ya wimbo wa Naitwa Roma”

“Kipindi ulivyotekwa mimi binafsi sikulala siku mbili tulikuwa tunashinda polisi Oysterbay, Mama Roma akasema hataki tena uimbe muziki, ukiwa unanishauri muda mwingine usijifanye ni mlokole sana unaimba nyimbo za gospel kuhusu huu wimbo wa Mungu yuko wapi wewe hukutakiwa kutia neno coz wewe ni mwana sana”

“nakushauri tu mwanangu fanya urudi watu watapita na mkeo, hakuna mwanamke anayeweza kuvumilia kukaa mwaka mzima bila kujamiiana, hao wanawake walishakufaga enzi za mababu zetu, kama unampenda mkeo na watoto fanya urudi hakuna mtu wa kukukamata mambo ya wimbo yalishapita” ameandika Nay wa Mitego