Advertisements

Mwanasiasa nguli wa upinzani kutokea Chadema Tundu Lissu amezungumzia kuhusu safari yake na hatari anayoiona juu ya usalama wa maisha yake huku akiwa anarejea nchini.

Lissu amesema hayo alipokuwa akizungumza na Watanzania kwa njia ya mtandao akiwa ughaibuni kuhusu safari yake ya kurudi Tanzania ambayo anatarajia kuianza hivi karibuni.

BOFYA USOME PIA…

“Wale watu waliokuja kuniua siku ile ya tarehe saba septemba miaka mitatu iliyopita na muliowatuma au waliowalipa au waliowaelekeza bado wanaitwa watu wasiojulikana maana yake ni kwamba hao watu bado wapo na kama wapo na hawajasema kama lengo lao ni kuniua wameliacha bado kuna hatari juu ya maisha yangu” Alisema Lissu

“Kwahiyo ninarudi nchini kwangu katika mazingira ambayo hatari dhidi yangu haijaondoka bado, Lakini ninarudi tu ni nyumbani kwetu, inabidi nirudi tu” aliongeza.

Kwa mujibu wa Mwanasiasa huyo amesema kuwa miezi sita iliyopita, Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe aliandika barua mbili kwenda kwa vyombo vya ulinzi na Usalama Tanzania ili kuomba apewe ulinzi pale atakaporejea Tanzania.

Advertisements

Anasema kuwa hadi sasa bado wanasubiri majibu kutoka kwa vyombo husika kwa hivyo ndivyo vina jukumu la kuhakikisha yupo salama baada ya yeye kurejea.

Lissu anatarajiwa kurejea Tanzania ifikapo Julai 28 akiwa kama mmoja wa walioomba kuteuliwa na chama hicho ili kuwania kiti cha urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.