Advertisements

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ameridhia uwanja wa Taifa kuitwa ‘Mkapa Stadium’ kufuatiwa na maombi ya wadau wengi wa michezo kuomba uwanja huo ubadilishe jina ili kumuenzi Rais mstaafu awamu ya tatu Mh Benjamin Mkapa.

Rais Magufuli ameridhia hivyo akiwa anahutubia Taifa katika siku ya Kitaifa ya maombolezo ya siku za mwisho kuuaga mwili wa Hayati Mkapa,

Rais Magufuli amesema kuwa Mzee Mkapa alitoa mchango wake katika kila sekta ya michezo na sanaa, na Watanzania hawatomsahau kwa kujenga uwanja huo wa Taifa.

SOMA ZAIDI…

“Mzee Mkapa aliujenga uwanja huu mkubwa wa michezo, kwa sasa wengi wanataka uwanja huu uitwe Mkapa Stadium”

Rais Magufuli ameeleza kuwa amekuwa akipokea meseji nyingi zikitaka uwanja huu uitwe kwa jina la Mkapa ingawa anafahamu kuwa Mkapa hakupenda kuita vitu vingi kwa jina lake, lakini kwa kuwa ameshalala hapa sasa anatamka rasmi uwanja huo kuitwa wa Mkapa

Advertisements

“Mzee Mkapa ameshafanya mengi kwenye sekta ya michezo, na ni kwasababu aliipenda michezo pia naambiwa alikuwa shabiki wa Yanga ingawa sikuwahi kumsikia akisema hadharani, Mzee Kikwete ananiambia hapa ni kweli alikuwa shabiki wa Yanga maana Kikwete ni shabiki wa Yanga, Sijui Mwinyi ni timu gani”