Advertisements

Malkia wa muziki wa Pop kutoka Marekani, Katy Perry amefunguka kuhusiana na jinsi ugonjwa wa Sonona ulivyokuwa ukiathiri mfumo wake wa maisha ya kawaida hali ambayo ilimfanya kuhisi kuwa asingeliweza kuuona mwaka 2018.

Mwimbaji huyo ambaye sasa hivi anatarajia kujifungua mtoto wake wa kwanza kwa mpenzi wake Orlando Bloom amezungumza kupitia jarida la Sunday Times kuwa ilifikia wakati ambapo alitakiwa kuanza matibabu ya ugonjwa wa akili.

Katy pia ameeleza kuwa hali yake ilizidi kuwa mbaya alipokuwa akifanya matamasha ya albamu yake ya tano iliyoenda kwa jina la The Witness “Huwezi kumbadilisha mtu kwa kiasi ambacho unahitaji nilihitaji kufanya maamuzi baada ya kufikia hatua mbaya” amesema mwimbaji huyo.

Advertisements

“Sikuwa na chaguo lingine isipokuwa kupitia katika hali hii ya kihisia, kiroho na kisaikolojia ambapo niliishi bila matumaini ya kuuona mwaka 2018, nilijaribu matibabu ambayo ndiyo yalisaidia sana” ameongeza Katy Perry.

Aidha Katy amebainisha kuwa kwa sasa ameweza kushinda na kuondokana na hali hiyo na hiyo ndiyo imekuwa maana halisi ya albamu yake mpya ya SMILE .

Katy ameongeza pia kuwa kwa sasa anajiandaa kujifungua mtoto mwenye afya njema na hayupo tena kwenye matibabu ya sonona.

Advertisements
Advertisements
Advertisements
Advertisements

All photos are credited to hollywood.com