Muigizaji kutoka nchini Marekani, Dwayne Johnson maarufu kama ‘The Rock’ ametangazwa kuwa muigizaji ambaye amelipwa pesa nyingi zaidi duniani kwa mwaka 2019.

Advertisements

Ikiwa ni kwa mara ya pili sasa Forbes inamtangaza The Rock kuwa mwigizaji ambaye anaingiza mkwanja mrefu sana Hollywood ambapo orodha ya mwaka 2018 alitangazwa kuwa nafasi ya pili huku orodha hiyo ikiongozwa na George Clooney, na sasa yeye ndiye amekuwa wa kwanza akiingiza kiasi cha Dola Milioni 85.7 za Kimarekani.

Bofya hapa kuona list>>> Orodha ya waigizaji wanaolipwa fedha nyingi duniani ‘Forbes’

Advertisements

Forbes wameeleza kuwa asilimia kubwa ya fedha hizo zimetoka kwenye filamu ya Red Notice ambapo The Rock ameshiriki kama Polisi wa Interpol, filamu hiyo imemuingizia Dola Milioni 23.5 za Kimarekani.

Dwayne Johnson ‘The Rock’
Advertisements

Pia filamu zingine ambazo zimemuingizia fedha ni Fighting with my family, Fast and Furious Presents: Hobbs and Shaw pamoja na Jumanji: The next level.

Rekodi hiyo inamuweka The Rock katika nafasi ya juu zaidi kwa watu mashuhuri ambao wanalipwa pesa ndefu sana katika mtandao wa Instagram akiwa analipwa Dola Milioni 1 ili kutangaza biashara ama brand yoyote akifuatiwa na Kylie Jenner ambaye analipwa Dola 986,000 za Kimarekani.

Soma pia>>> Kylie Jenner ‘hakuna tofauti kati yangu na Kim Kardashian’

Kabla ya The Rock kutangazwa kama mwigizaji anayelipwa pesa nyingi, Kylie Jenner ndiye aliyekuwa anaongoza kwa kuingiza fedha nyingi kupitia mtandao wa Instagram.

Advertisements