Mtayarishaji wa muziki Swizz Beatz ambaye pia amehusika katika kutayarisha albamu hiyo amevunja ukimya kwa kuwaambia mashabiki sababu ambazo zimepelekea Diamond kuimba kiduchu kwenye nyimbo hiyo.

Moja kati ya komenti ambayo imewekwa na Swizz Beatz kwenye uwanja wa komenti kwenye ukurasa wa instagram wa Alicia Keys imesomeka kuwa “My brother for life please let your fans know you did as you pleased on the record and this is just part one” katika komenti hiyo Swizz Beatz alimaanisha kuwa Kaka yangu wa damu au maisha tafadhali uwaambie mashabiki zako kuwa kile ambacho ulikifanya ni sehemu ya kile ulichotaka kukifanya na hii ni sehemu ya kwanza tu.

Albam hiyo ya saba kwa mwanamama huyo iliyoenda kwa jina la stylized in all caps imeachiwa tarehe 18 Septemba 2020

Advertisements

Get new content delivered directly to your inbox.

Advertisements