Baada ya kufanya kolabo na nyota wa muziki nchini Diamond Platnumz, Kolabo iliyokwenda kwa jina la “Shusha” Official Baba levo amekuwa msanii ambaye ameweka headlines nyingi sana ambazo zimemuonyesha waziwazi akimkingia kifua Diamond Platnumz na hivi karibuni atangaza vita kwa mtu yeyote atakayemtukana Diamond.

“Natangaza rasmi ukimsema Diamond vibaya ujue umeingia kwenye vita rasmi na mimi, sijali waniite chawa, kunguni au papasi cha msingi ni boss wangu na ananilipa mshahara wa mamilioni” amesema Baba Levo

Maneno hayo ameyatoa babalevo akiwa kwenye mahojiano na kituo cha Wasafi Fm, pia ameongeza kuwa Diamond Platnumz ameweza kugharamia video yake ya “Shusha” kwa zaidi ya shilingi Milioni 28 za Kitanzania bila ya kudai kurudishiwa hata senti Tano

Hivyo Baba Levo amechukulia kitendo alichokifanya Diamond Platnumz kwake ni mapenzi makubwa aliyonayo kwake kimuziki na maisha ya kawaida.

Soma zaidi..

Swizz Beatz afunguka sababu za Diamond kuimba Kiduchu kwenye Wasted Energy
Diva ashusha nzito kwa Kiba ‘Kigagula sikulipenda’
Stunning pics of Diamond Platnumz, show off