Watu wengi hawamuelewi nyoka pamoja na jinsi ya kujikinga naye ili asikudhuru au namna ipi ni sahihi kufanya ili kupunguza makali ya sumu ndani mwili wako.

Mara nyingi viumbe aina ya nyoka huwa hawamkimbizi binadamu kwa maana ya kutaka kumdhuru bali kwa namna ya kujilinda dhidi ya binadamu hao, Shirika la Afya linasema kuwa “watu takribani milioni 5.4 huwa wanaumwa na nyoka kila mwaka, huku watu takribani milioni 2.7 huumwa na nyoka ambao wana sumu kali mno”.

Hata hivyo Shirika hilo linazidi kuripoti kuwa kati ya watu 81,000 hadi 138,000 huwa wanakufa kila mwaka kutokana na kuumwa na nyoka pamoja na kuchelewa kwa huduma ya kwanza ambayo hupelekea kusambaa kwa sumu ya nyoka ndani ya miili yao na hatimaye kupoteza uhai.

Advertisements

NAMNA YA KUTOA/KUJIPA HUDUMA YA KWANZA BAADA YA KUNG’ATWA NA NYOKA

Hizi ndizo hatua, njia au tahadhari 8 za kuzingatia/kuchukua pindi unapong’atwa na nyoka ili kujikinga na madhara mabaya zaidi.

Advertisements
  1. Jambo la kwanza kabisa ni kutulia au kumtuliza mgonjwa aliyeumwa na nyoka kwani jambo hili hufanya mapigo ya moyo kwenda taratibu na hivi kupunguza kasi ya mzunguko wa damu mwilini, Sumu ya nyoka inapoingia mwilini huweza kusambaa kupitia damu hivyo kupunguza kasi ya mzunguko wa damu ni kupunguza kasi ya kusambaa kwa sumu mwilini.
  2. Ondoa vitu vyote vinavyoweza kuzuia mzunguko wa damu katika mwili wa muhanga kama vile saa, mkanda, pete na viatu kwani vinaweza kumletea matatizo
  3. Safisha eneo lililong’atwa, hakikisha usichue wala kulisugua kwa kitu kigumu kwani unaweza kusababisha sumu iliyoko nje kuingia ndani.
  4. Mzuie mgonjwa asitembee hovyo hovyo, kugaragar ama kuleta purukushani yoyote, kama utaweza mbebe kumpleka hospitali au omba msaada ulio karibu yako,
  5. Funga bandage na weka pressure kwa juu la jeraha ili kuzuia damu yenye sumu isielekee upande wa moyoni.
  6. Usimpe mgonjwa kimiminika cha aina yoyote, maji, juice, au pombe kwani vinaweza kumlete madhara zaidi
  7. Usikate sehemu iliyong’atwa na kufyonza kwani hakuna uthibitisho wa kisayansi unaosema kufanya hivyo kunaweza kupunguza kasi ya kusambaa kwa sumu mwilini mwa aliyng’atwa bali kunweza kuleta madhara zaidi kwa anayefyonza sumu hiyo.
  8. Mwisho elimu kubwa itolewe kwa wafugaji pamoja na wakulimu wa mashambani kwao wao ndio kwa ukubwa watu ambao wanatumia muda mwingi wakiwa katika maeneo ambayo ndio kama maskani mwa nyoka.

Fahamu zaidi