Yaliyomo nyuma ya pazia, nyimbo ya Satan ya Rosa Ree na jinsi inavyogusa hadithi ya mahusino yake ya kimapenzi

Muziki wa hip hop ni miongoni mwa miziki ambayo inastrugggle sana ili kupenya kwenye soko la muziki nchini ukilinganisha na ilivyo kwa bongo fleva ijapokuwa wasanii wake wanafanya vizuri hususan kwenye utungaji wa mashairi yao ambayo mingi sana hugeuka kuwa msemo mtaani.

READ MORE

hivi karibuni wasanii wa hip hop wamegeukia sana soko la muziki kwa albam ambayo hivi sasa ndio imekuwa kama mpango kazi namba moja ambao utakufanya uonekane msanii bora kwenye soko la muziki.

Leo tumzungumzie msanii ambaye amekaa kwa muda mrefu kwenye game ya hip hop nchini (ROSA REE) pamoja na wimbo wake ambao tangu utoke umekuwa gumzo huku mtaani, wimbo wa Satan.

Ukiusikiliza wimbo huu kwa akili ya kawaida au kuutazama kwa macho ya kawaida utaona ni wimbo Rosa Ree ameuimba kwa uchungu sana jinsi alivyokuwa akifoka maneno yake, picha zilizomo lakini hata midondoko ya beat ya ule wimbo yote inaonyesha hali ya uchungu mno.

Pia maudhui ambayo yamo kwenye nyimbo ya Satan, yanaonyesha kuwa ukiachana na mambo yote ambayo muimbaji anapitia/amepitia bado anamkataa shetani, anakataa kuwa mfuasi wa shetani. Kuna mstari ambao Rosa amesikika akisema

Cos none of my attention should ever be given to you, i will never be your disciple

Rosa Ree
Advertisements

Lakini kama ilivyo ada kwa sanaa mara zote huwa ni yaleyale yanayoizunguka jamii ndiyo yanayoimbwa kuigizwa ama kutungiwa kazi yoyote ya kisanaaa, swali kubwa hapa ni kwamba haya yote aliyoyaimba Rosa ni mambo ambayo amepitia yeye mwenyewe, mtu/watu wa karibu au jamii anayoishi?

Hivi karibuni Rosa amepost video ambayo imeonekana kuwa kielelezo namba moja cha kwanini aliamua kutulia chini na kandika ngoma ya satan, ndani ya clip hiyo ameeleza hadithi ya uchungu katika mahusiano aliyopitia jinsi alivyokuwa akionewa na aliyekuwa mpenzi wake, jinsi alivyopigwa na kufungiwa ndani ya chumba pia kuzibwa mdomo asiweze kupigwa kelele.

Pia Rosa ameeleza kwamba hata alipopata nafasi ya kutoroka kwenye chumba hicho na kuomba msaada basi watu hawakumjali na wakahisi kuwa kwakuwa ni suala la mahusiano basi haliwahusu jambo ambalo yeye amelichukulia kama mtazamo hasi, kwani yoyote anayehitaji msaada ni vizuri akisaidiwa.

Mwishoni mwa video hiyo Rosa amewasihi watu kutokata tamaa katika magumu wanayopitia kwani kukata tamaa ni sawa na kumpa shetani nafasi ya kutimiza mipango yake kwako.

Advertisements

Kwangu mimi, ningependa kumpa big up sana Rosa kwa hatua ambazo anapiga kwenye muziki wake lakini pia kuwaonyesha watu kuwa hata walio mastaa pia wana majanga yao ambayo wanayapitia tena wakati mwingine huwa ni makubwa zaidi hata watu wa kawaida hivyo wanapohitaji msaada tuwasaidie tuweke muonekano wao pembeni kisha utu utawalee.

Thanks #Mtazamo.