Mkubwa Fella ametoa la moyoni mwake kwa Watanzania alipokuwa akihojiwa na Bongo5, meneja huyo amesema kuwa , kama Watanzania tunapaswa kuwa wamoja pale linapokuja jambo la Kitaifa mfano “Tuzo”

“Mimi siku nikimuona mtu ana jambo la kitaifa hata awe adui gani upande wangu, lazima nimpost na nimuombee naomba tumpe-support mwana huyo” alisema Mkubwa Fella.

Maneno hayo ya Mkubwa Fella yamekuja hivi karibuni baada ya Nyota wa muziki kutoka WCB, Diamond Platnumz kuchaguliwa kushiriki kuwania tuzo ya Best International Act ya BET Awards.