News Tips

Fahamu alichokisema Mkubwa Fella kwa wasanii wa Tanzania hivi leo

Mkubwa Fella asisitiza umoja kwa wasanii hasa kwenye mambo ya Kitaifa

Ona jinsi panya wa Tanzania wanavyoweza kutegua mabomu yaliyotegwa ardhini

Tanzania: Panya anayeweza kugundua mabomu yaliyotegwa ardhini, atuzwa

China hivi sasa imewaruhusu raia wake kuzaa watoto kufikia hadi watatu baada ya kupungua kwa idadi ya watoto wanaozaliwa nchini humo, hatua ambayo inakdiriwa kuwa ni mabadiliko makubwa ya sera nchini humo

https://pagead2.googlesyndication.com/pagead/js/adsbygoogle.js?client=ca-pub-2897539933935547 (adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});

Hatua hiyo imetangazwa siku ya jumatatu na serikali ya China katika mkutano uliofanywa na viongozi wakuu wa chama cha kikomunisti.

Tangazo hili limekuja baada ya matokeo ya hesabu za watu nchini humo ambayo hufanyika kila baada ya miaka 10 kurekodi idadi ndogo ya ukuaji na hivyo kupelekea Beijing kubatilisha sheria yake ambayo inamtaka kila Mchina kuwa na mtoto mmoja mpaka wawili tu.

Gharama za kulea watoto nchini humo zimefanya wanandoa wengi kushindwa kuzaa watoto wengi zaidi, Hatua iliyoafikiwa na viongozi wakuu pia imeidhinishwa na Rais XI Jinping katika mkutano wa viongozi hao wa kisiasa limesema shirika la habari Xinhua.

Advertisements

Mkubwa Fella asisitiza umoja kwa wasanii hasa kwenye mambo ya Kitaifa