Hivi karibuni polisi katika wilaya ya Moroto kaskazini mwa Uganda wameanza kuwasaka watu wanaonunua chapati 5 au zaidi kwa madai ya kuwa huenda watu wao wakawa wanawalisha wezi wa mifugo eneo hilo

Msemaji wa Polisi Michael Longole amenukuliwa akizungumza na Stesheni ya Uganda Radio Network kuwa ” Tumepokea taarifa kuwa wale wanaonunua chapati nyingi wanawapelekea wapiganaji msituni”

Alisema zaidi kuwa kukomesha usafirishaji wa chakula kwa wezi hao huenda kukawalazimisha kutoka mafichoni na kusalimisha silaha zao

Mwanaharakati wa amani eneo hilo, Mark Koryang alisema kuwa mpango huo hautaweza kufaulu kwani wapiganaji hao wanaweza kuishi bila kula chapati, mwingine alisema kuwa maafisa wa usalama nchini Uganda wanahitajika kufanya kazi kwa ukaribu na wananchi wa eneo hilo ili kuweza kukabiliana na ukosefu wa amani katika eneo hilo.