Msanii wa Bongo fleva kutoka katika kundi la Konde Gang, Ibraah ametupa dongo kwa Rayvanny baada tu ya kuichukua nafasi ya kwanza on Trending kupitia Youtube ambayo hapo awali ilikuwa ikishikiriwa na Rayvanny (lecturer) na wimbo wake aliokuwa amemshirikisha Whozu.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Ibraah aliandika kuwa, “Lecturer somo limemshindwa vumbi tu am young and genius number one”

Maneno haya yameonekana kumlenga Rayvanny kwani ndiye mwanamziki pekee ambaye alijipa jina hilo hivi karibuni alipokuwa akiupromote wimbo wake, mara baada tu ya Harmonize kujitangaza kuwa yeye ndiye #Teacher wa muziki wa amapiano.

Aidha Harmonize ameonekana kutopendezwa na kejeli hizo zilizotumwa na Ibraah baada ya kuamua kumjibu msanii wake “Kwa faida Ya Sanaa Ya Tanzania na Vizazi Vijavyo Nisingependa kuwaona Mnagombana naaamini Wote ni Vijana na mna Ndoto Isitoshe family’s Zinawategemea FANYA MUYAMALIZE MATATIZO YENU. BINAFSI SIPENDEZEWIIII kila mtanzania Halisi Anawategemea kesho Mje kuipeperusha hiii BENDERA 🙏”