Bantu ni filamu ya kibongo ambayo imeandikwa na kuwa directed by Freddy Feruzzi ipo katika muundo wa series na episode yake ya kwanza imejikita kuzungumzia vijana wawili ambaye ni Jishu pamoja na rafiki yake wanaopambana kuiangamiza familia ya kifalme kwa madai ya utawala mbovu na wa kidharimu
Mwanzo kabisa anaokena mdada ambaye huko mbeleni anatambulika kama mlinzi wa pekee kwa Malkia Sheba na anaonekana akiwa nafanya maombi ya kusafiri salama kuelekea Kizwe.
Kisha anaonekana Jishu pamoja na rafiki yake wakiwa mzee mmoja ambaye walikuwa wakimlazimisha awaoneshe njia ya kumpata Malkia sheba japo alikataa na wakamua kumuua kisha kuendeleza msako wao wa kumtafuta Malkia sheba
baada ya muda walikuja kumuona na hapo ugomvi ukatokea kati ya Jishu na rafiki yake dhidi ya Mlinzi wa Malkia Sheba na baada ya Muda Mlinzi anaonekana kuzidiwa.
YOU CAN WATCH IT HERE
Jishu anafanikiwa kumfikia Malikia na hapo utaona malkia akivua pete yake ya mkononi na kumpa Jishu. Lakini wakati malkia anampa pete jishu mlinzi wa malkia ambaye alikuwa amelala chini akiugulia maumivu anaonekana akiamka na kwenda kumchoma kisu Jishu, na filamu hii ikaishia hapo hivyo hatujui kama Jishu atakufa au la so I hope episode inayofuata itaenda kuelezea zaidi nini kinafuata
WHAT TO KNOW?
Kwanza kabisa sauti za waigizaji kwenye filamu hii zinasikika vizuri sana, huwezi kupata shida yoyote ya sauti pindi unapokuwa unaangalia filamu hii.
Picha na Rangi za filamu hii ni nzuri na madhari yake iliyotumika inavutia mno
Lakini kuna baadhi ya mambo ambayo huenda yamefichwa na mpaka episode ijayo ndipo yakajulikana zaidi mfano, Mzee ambaye ameuwawa na Jihu wakati filamu inaanza hatuwezi kujua ni baba wa Malkia sheba au ni mwananchama tu wa familia ya kifalme yaani royal family
Pia bado Malkia Sheba haijulikani anatokea wapi isipokuwa tunajua tu kuwa anaeleka kizwe ambako hatujui kama huko ndiko ufalme wake uliko au la, hili ni swali ambalo litaenda kujibiwa na episode zinazofuata.
Scene ya mwisho pia tunaweza kumuona malkia akiwa anavua pete na kumkabizi Jishu ambaye kwa pale tunaewza kusema kama ni adui yake so, episode wone haijweka wazi kuwa ile pete ina mamlaka gani na kwa nini anampa perhaps episode zinaazofuata inaweza kuwekwa wazi.