Wakati wa utengenezaji wa filamu matukio mengi hutokea na mengine huwa ya kweli na mengine huwa ya uongo, muigizaji kutoka Marekani anayefahamika kwa jina la Alec Baldwin amejikuta akisababisha kifo cha mwanamke aliyefahamika kama Halyina Hutchins ambaye alikuwa mpiga picha katika sinema hiyo baada ya kufyatua risasi kwa kutumia bunduki ya maigizo.

Aidha katika tukio hilo pia mwanaume mmoja amejeruhiwa na tayari amefikishwa hospitalini kwa matibabu zaidi,

Polisi katika jimbo hilo la Marekani walisema Bwana Baldwin alitumia silaha hiyo katika utengenezaji wa filamu mpya ya Rust ambapo seti hiyo ilikuwa ikizungumzia matumizi mabaya ya bunduki ya maigizo.

Bwana Baldwin ameandika kupitia ukurasa wake wa twitter akieleza jinsi alivyosikitishwa na kutokea kwa jambo hilo