Kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania Dkt, John Pombe Magufuli kimesikitisha watu wengi huku kikiliacha taifa katika simanzi, huzuni na giza nene lenye fumbo ndani yake.

Viongozi pamoja na watu mashuhuri wametoa kauli zao kufuatiwa na kifo hiki huku wengi Watanzania wengi wanaofuatilia mitandao kwa ukaribu wakishangazwa na ukimya uliopo kwa aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda kwani tangu kifo kitokee hakusema neno lolote bali alikaa kimya.

Advertisements

Baada ya kusambaa kwa picha ambazo zimemuonesha akiwa mmoja wa waudhuriaji wa msiba wa Hayati Dk Magufuli, Mhe Makonda ameamua kuvunja ukimya kwa kuandika kupitia ukurasa wake wa Instagram maneno ambayo yanasomeka hivi.

“Pamoja na kukuona jana bado moyo wangu unaamini umelala hujafa. Rafiki , kaka na Kiongozi wangu utakapo amka usingizi kuna jambo nitakwambia”

Mhe Paul Makonda