Je wajua?: Haiti na Liechtenstein ndizo nchi mbili zilizowahi kutumia bendera  zinazofanana katika mashindano ya Olimpiki.

Bendera ya Taifa huwakilisha mambo mengi yaliyomo katika taifa husika, yaweza kuwa imani katika taifa hilo, rangi ya watu wa taifa hilo na pia hata utajiri uliopo katika taifa hilo

Si kawaida kuona bendera za nchi mbili tofauti zikifanana kwa rangi amA nembo, kwani kila nchi ina ustawi na utajiri wa aina yake hivyo inashangaza sana endapo jambo kama hili linapotokea.

Kwa kipindi cha muda mrefu Haiti na Liechtenstein zimekuwa zikitumia Bendera zinazofanana kwa rangi pia zilizoundwa kwa muundo unaofanana, yaani rangi nyekundu ikiwa kwa chini na rangi ya buluu ikiwa kwa juu.

Mnamo mwaka 1939 majira ya joto, katika mashindano ya Olimpiki nchi ya Haiti na Liechtenstein baada ya mashindano kuanza ndipo ikagundulika kuwa wanatumia bendera zenye kufanana kwa rangi na pia muundo wake.

Baada ya kutambua hilo nchi hizi mbili ziliamua kuongeza nembo ambayo ingekuwa kama alama ya utofauti wa Bendera zao, na mpaka leo bendera za nchi hizi mbili zinafanana katika rangi lakini nembo tofauti.

Je Wajua?: Saudi Arabia ni moja kati ya Nchi 19 ambazo hazijapitiwa na mto wowote duniani.

JANGWA LA SAUDI

Saudi Arabia ni moja katika ya falme za kiarabu zenye kumiliki utajiri mkubwa sana duniani lakini pia ni nchi ya tano kwa ukubwa katika bara la Asia, katika dunia nzima Saudi Arabia ndiyo nchi kubwa pekee ambayo ndani yake haijapitiwa na mto wowote.

Aidha, ndiye nchi ya pekee katika dunia ambayo imebarikiwa kuwa na  ghuba ya Persia na mwambao wa Bahari Nyekundu kwa pamoja.

Orodha ifuatayo inayonesha nchi ambazo hazijapitiwa na mito yeyote

Rank Countries Without Rivers
1 Bahamas
2 Bahrain
3 Comoros
4 Kiribati
5 Kuwait
6 Libya
7 Maldives
8 Malta
9 Marshall Islands
10 Monaco
11 Nauru
12 Oman
13 Qatar
14 Saudi Arabia
15 Tonga
16 Tuvalu
17 United Arab Emirates
18 Vatican City
19 Yemen

Kwa taarifa zaidi, SUBSCRIBE katika tovuti hii…