Je Wajua? Hadithi ya Blanche, msichana aliyefungwa ndani ya chumba kichafu, chenye giza totoro kwa muda wa miaka 25?

Blanche Monnier msichana aliyefungwa kwa siri na mama yake  ndani ya chumba kidogo chenye giza totoro kwa muda wa miaka 25.

Kisha akaja kukutwa na polisi akiwa katika hali duni, aliyekonda na kuchakaa kabisaa, kwa mujibu wa ripoti za Polisi hao walisema kuwa Monnier hakuwahi kuona mwanga wa Jua kwa muda wote alipokuwa amefungwa.

Hadithi hii iliyojaa mengi ya kustaajabisha na kuhuzunisha inaanzia mnamo mwaka 1849 huko Poitieres, Ufaransa ambako alizaliwa Blanche Monnier katika familia ya kitajiri, Blanche alikua katika uzuri na mvuto wa sura na hata alipofikisha umri wa miaka 25, maajabu ya uzuri wake tayari yalishaanza kuonekana kwani wachumbiaji wengi kutoka katika familia za kitajiri walianza kujitokeza kutaka kumchumbia.

Blanche hakuwa tayari kumkubalia mtu yeyote aliyejitokeza kwenda kumchumbia kwani moyo wake tayari ulishafungwa katika penzi la Mwanasheria.

Ulipofika mwaka 1874,  Blanche aliamua kumtambulisha mchumba wake kwa mama yake aliyejulikana kama Louise Monnier, ili apate ruhusa ya kufunga naye ndoa, jambo hili halikumfurahisha mama yake alihisi kama bintiye kuolewa na mwanasheria ni kudhalilisha ukoo wao wa kitajiri.

Ndipo alipomuonya Binti yake kuwa asingeweza kuolewa na mwanasheria na kama anataka ndoa basi anapaswa kumkubali mmoja kati ya vijana waliotoka katika familia ya kitajiri, Blanche hakuweza kukubaliana na mama yake katika jambo hili.

Kutokana na Blanche kuwa mbishi katika kukubaliana na maamuzi ya mama yake, ndipo mama huyo alipoamua kumfungia mwana wake katika chumba ambacho ni kidogo, chenye giza tena hakikuwa safi kwa matumizi ya binadamu,

Soma pia: Je Wajua? Mchoro wa Monalisa ulipata umaarufu duniani baada ya kuibiwa kwake

Louise Monnier n kaka yake aliyeitwa Marcel walitangaza kifo cha Blanche Monnier kisha zikatengwa siku kwa ajili ya maombolezo ya kifo chake, kitu cha kusikitisha ni kwamba hata marafiki zake wa karibu hawakuweza kutambua nini kinaendelea kuhusiana na kifo feki cha rafiki yao Blanche.

Hata mpenzi wake, mwanasheria aliyependwa na Blanche kwa dhati hakuweza kutambua ni jambo gani limepelekea mpenzi wake kupoteza uhai wake kama ilivyokuwa imetangazwa. na ilipofika mwaka  1885 alipoteza alifariki dunia .

“Hakuna siri itakayofichwa milele, kila kilichofichwa kitavumbuliwa”  ilipofika  23 Mei 1901 Wakili Mkuu a Paris alipokea barua kutoka kwa mtu asiyejulikana (anonymous source) iliyompa maelezo kamilifu juu ya mwanamke ambaye amefungwa kwa miaka 25 ndani ya nyumba ya Louise Monnier akiishi katika mateso na taabu.

Jambo hilo lilimstua Sana wakili huyo mwishowe akaamua kuomba kikosi cha Polisi kwa ajili ya upelelezi zaidi,

Walipofika ndani ya nyumba ya Louise Monnier walifuata maelekezo ya barua ambapo iliwafikisha moja kwa moja katika chumba alichokuwa amefungwa Blanche Monnier.

Kwa wakati huo Louise mwenyewe alikuwa ametulia kimya ndani ya chumba chake na kaka yake Marcel, akiwa bado anaishi ndani ya nyumba hiyo, jambo ambalo inaonesha kuwa Mama huyo aliweza kumhadaa kijana wake wa kiume asiweze kwenda kuishi mahala popote mbali na nyumbani.

Waligonga mlango wakiwa na matumaini ya kusikia sauti yeyote ya majibu, la hasha! haikuwa hivyo japo waliweza kusikia sauti ya mjongeo kutoka ndani ya kile chumba.

Baada ya jitihada za kugonga mlango kugongwa mwamba waliamua kuvunja mlango na kuingia ndani kwa lazima.

Jarida la History Collection linaandika kuwa walipoufungua mlango walistaajabu kuona skeletoni ambalo limefanana na Monnier, limejifunika blanketi kwa uwoga.

Picha kutoka mtandaoni ikimuonesha Blanche baada ya kufungwa ndani kwa miaka 25

Polisi walipomuangalia vizuri waliweza kutambua kuwa ndiye Monnier mwenyewe akiwa katika hali mbaya, anatoa harufu kali tayari alikuwa ameshafikisha miaka 50, huku miaka 25 akiwa anaishi bila ya kuliona jua.

Blanche Monnier alikutwa akiwa uchi kama alivyozaliwa, alikuwa mwoga tena alionekana kuwa mwenye kushangaa sana, kwa haraka alianza kuchukuliwa vipimo vya uzito na akapatikana akiwa na kilogram 25 tu.

Polisi walipofanya uchunguzi zaidi waliweza kugundua mabaki ya chakula yaliyooza na wadudu ndio waliotawala chumba kile, hakuna hata mtu mmoja aliyejishughulisha kufanya usafi kwa ajili yake.

Blanche alichukuliwa na jopo la madaktari kisha kwenda kupatiwa matibabu katika hospitali ya Hotel-Dieu, japo madaktari wengi walifikiri Blanche asingeliweza kuishi kwa muda mrefu haikuwa hivyo, alianza kupatiwa huduma zote kama binadamu wa kawaida japo mwanga wa jua kwa wakati huo ndio ulikuwa adui namba moja kwake.

Jambo hili halikuishia hapo, Marcel akiwa na Mama yake walikamatwa na kufikishwa mahakamani kwa mashitaka mbalimbali yanayohusiana na kumfunga mtu bila kibali, Cha ajabu ni kwamba kila walipoulizwa kuhusu kwanini walifanya hivyo,

Marcel Monnier, kaka wa Blanche alijibu kuwa Dada yake alikuwa mwanamke mwenye hasira sana, hivyo waliamini kuwa Blanche angekuwa na ugonjwa wa akili, na kuhusu kufungwa kwa miaka 25, ni yeye mwenyewe ndiye aliyechagua kufanya hivyo ili asiweze kuolewa na mtu yeyote.

Pia : Je Wajua?: Nchi mbili zilizowahi kutumia bendera zinazofanana

Hivyo isingekuwa vizuri kwao kumnyima haki yake ya kufungwa katika chumba hicho, aliongeza akisema kuwa, Dada yake hakuwahi kujaribi kutoroka kutoka katika chumba hicho bali alikubali hali hiyo kisha akatulia humo kimya.

Maelezo haya yalikataliwa na mahakama kuwa si ya kweli, baada ya majirani walioishi maeneo hayo kuja mahakami kutoa ushuhuda wa kile walichokuwa wakikisikia.

Wengi wao walisema kuwa kila walipopita karibu na maeneo ya nyumba ya Monnier waliweza kusikia sauti ya mwanamke akipiga kelele “Polisi…Polisi” kutokea katika dirishani lililozibwa kwa mbao akiomba msaada.

Blanche baada ya kupelekwa hosptali hakuwa mgomvi wala kuonyesha tabia za ajabu bali alikuwa akiwashukuru madaktari kwa kumtoa katika giza nene, japo jambo lililoumiza moyo wake ni kwamba hakuwahi kumuona mpenzi wake kwani tayari alikuwa amefariki dunia.

Mama yake alikutwa na hatia,  kisha akapelekwa jela baada ya hukumu kusomwa, lakini kutokana na uzee aliokuwa nao aliweza kufariki dunia siku 15 tu baada ya kuhukumiwa.

Kaka yake alihukumiwa mwaka mmoja jela, lakini naye pia alikuwa hakimu hivyo alifahamu mbinu za kujitetea na kujilinda hivyo alitumia taaluma yake na akafanikiwa kuondokana na kifungo hiko cha mwaka mmoja.

Blanche Monnier alikaa hospital kwa muda baada ya kuwa sawa kiafya alitakiwa kuruhusiwa, lakini hakuwa na mahali popote pa kwenda kuishi, hivyo aliomba kwenda kuishi kwani asingeliweza kwenda kuishi nyumbani na kaka yake katika hali ile hivyo alipelekwa kuishi katika hospital ya Blois Psychiatric Hospital  ambako alipoteza maisha mnamo mwaka 1913.

“Kama umeipenda hadithi hii tunakuomba kufollow Mira Magazine ili uwe wa kwanza kusoma hadithi na habari zetu”

“If you’re interested with this story we beg you to follow us, and you will receive the direct mail to your mailbox”

Chanzo cha habari hii ni..

University of Kentucky,Nineteenth Century French working Women: Love Marriage and Children

Also: The story of the French Socialite who was locked away for quarter of a century, 1976