AMERICAN idol imerudi tena katika msimu wa 18, huku ikiwa imepambwa na sauti za waimbaji wazuri zilizostaajabisha majaji.

Mwanaume mmoja anayefahamika kwa kazi yake ya usafi wa jiji (garbage man) amemfanya atokwe na machozi mwanadada  Katy Perry kutokana na uimbaji wake mahiri.

Mwanzoni mwa msimu mpya wa American idol, kila mgombea huwa na shauku kubwa ya kutaka kufanya vizuri ili kupanda mpaka simu unaofuata,

Mgombea Doug Kiker, Mfanya usafi kutokea jiji la Alabama, ambaye hakuwa na uzoefu mkubwa sana katika kufanya matamasha jukwaani aliweza kutingisha hisia za majaji baada ya kuimba kibao cha “God Bless the Broken Road”

Ilipofahamika kuwa Doug hakuwahi kupanda jukwaani kabla, aliombwa na nguli wa muziki wa taratibu, Lionel Richie kwenda kupewa mafunzo ya jinsi ya kufanya pale atakapokuwa jukwaani.

Akiwa anasubiliwa Doug, Binti wa miaka 16, Camryn Leigh Smith alipewa nafasi ya kuonyesha kipaji chake mbele ya majaji kwa kulitawala jukwaa la American idol huku akiimba vizuri wimbo wa Jessie J’s  ulioitwa “Big White Room”.

Baada ya kumaliza kuimba wimbo huo, Mwimbaji na mwandishi mashuhuri wa nyimbo za Pop, Katy Perry ambaye pia ni jaji katika tamasha hilo, alisema kuwa

“Camryn ni tumaini jipya katika msimu huu ni ndio kutoka kwa majaji wote”

alimalizia kwa kumpa ndio ambayo itamfanya aendelee kubaki katika msimu  wa 18 ndani ya American idol.

Baaada ya Camryn kushuka jukwaani alifuatiwa na Doug ambaye alipelekwa katika mazoezi ya muda mfupi jinsi ya kuliendesha jukwaa, Doug aliimba wimbo wa “God Bless the Broken Road” uliotungwa na Rascal Flatts.

Uimbaji wake wa pekee ulisaidiwa na jaji Luke ambaye alifanya kazi ya kupiga piano vizuri ili kuendana na tone aliyokuwa akiitumia Doug hapo jukwaani.

Alipomaliza kuimba aliwashukuru majaji wote kwa kumpa nafasi ya kuonesha kipaji chake ingawa ni kwa mara ya kwanza anafanya hivyo, alipomaliza kusema hayo Katy Perry alianza kudondosha machozi bila kutarajiwa.

“Umesimama wewe kama ulivyo, na utafika mbali sana wewe si mfanya usafi tena, bali ni ukuu ndani yako Tunakwenda Hollywood na wewe” alisema Katy Perry huku akitokwa na machozi.

Aliyefuata kuonyesha kipaji chake jukwaani hapo alikuwa ni kijana wa miaka 18 Francisco Martin, ambaye aliimba wimbo wa “Alaska’ ulioimbwa na Maggie Rogers.

#Appreciation to Hollywood life