Met Gala kama wengi wanavyopenda kuita hii sherehe ya harambee ambayo hufanyika kila mwaka tangu kuanzishwa kwake mwaka 1946 kwa ajili ya kupata pesa zitakazosaidia taasisi ya Sanaa ya Mavazi jijini New York. Harambee hii kila mara inapofanyika basi huashiria ufunguzi wa maonyesho ya taasisi ya mavazi  na huku kila mwaka maonyesho hayo hubeba ujumbe/dhumuni lake mahususi kwa mwaka huo.

Na mwaka 2021 Met gala imefanyika ikiwa na ujumbe wa American independence.

Tangu kuanzishwa kwake harambee hii imekuwa kinara katika harambee zote ambazo zimewahi kukusanya fedha nyingi sana kwa usiku mmoja na ikiwa imeweka rekodi ya kukusanya kiasi ya dola za kimarekani milioni 9 kwa mwaka 2013 na kuja kuvunja rekodi hiyo kwa dola za kimarekani milioni 12 kwa mwaka uliofuata.

Tangu kuanzishwa kwake wahudhuriaji wa harambee hiyo ni watu ambao wana hadhi za juu katika jamii hasa wale ambao wamefanikiwa katika Nyanja ya muziki, filamu, pamoja na fasheni.

Mwaka 2021 tiketi ya mtu mmoja kuhudhuria katika harambee hiyo ilikuwa ni dola za kimarekani takribani 35,000 ambayo ni zaidi ya milioni 80 za kitanzania huku meza moja ilikuwa ikigharimu kiasi ya dola laki mbili pia ni zaidi ya milioni 460 za kitanzania.

Hawa ni baadhi ya mastaa ambao walihudhuria wakiwa na mavazi yao ambayo yaliushangaza sana ulimwengu

Rihanna

Naye ni mmoja kati ya mastaa waliopendeza sana alionekana akiwa kwenye vazi lake ambalo ni kubwa na lenye rangi nyeusi huku akiwa na mkufu shingoni mwake pamoja na kitambaa cha almasi

Jennifer Lopez

Muonekano wake akiwa kwenye gauni la kahawia lenye mpasuo mkubwa ni kama vile cowgirl huku shingoni mwake akipigilia mkufu wenye umbo la V mkononi mwake alionekana ameshikiria koti jeusi lililotengenezwa kwa manyoya yenye  rangi nyeusi na hudhurungi na kichwa chake alikifunika kwa kofia nzuri ya kuvutia mno.

Kim Kardashian

Ukizungumzia mastaa ambao walishika trend kimavazi siku chache kabla ya tamasha hili kufikia kilele basi huwezi kumsahau kim Kardashian west pamoja na nguo yake ambayo imemfunika mpaka uso wake

Kendall Jenner

Naye alidamshi usiku akiwa na gauni kubwa ambalo limetengenezwa kwa crystals za kumeremeta ambazo hazikuficha mwili wake wote

Lil NaS x

Siku hii imeonekana kuwa nzuri sana kwa Lil Nas X kwani aliweza kudamshi akiwa na mavazi matatu tofauti na yote yakiwa ymeshavaliwa, yaani alichokuwa anafanya ni kuvua tu kila baada ya hatua aliyokuwa akipiga